Business

header ads

Maambukizi ya homa ya Ini yameongezeka kwa vijana wanaotumia dawa za kulevyaTakwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya homa ya ini kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya Jijini
Dar es Salaam, nchini Tanzania.


Akiongea jijini Dar es Salaam ,katika siku ya Maadhimisho ya Homa ya Ini duniani, Meneja mafunzo wa kituo cha madaktari wa ulimwengu wanaowahudumia watumiaji wa dawa hizo jijini Dar es Salaam ,Damal Lukas amesema katika wilaya ya Temeke kuna zaidi ya asilimia 18 na Kinondoni ni zaidi ya asilimia 70 ya vijana waliopimwa homa ya ini na kubainika kuwa na virusi vya homa hiyo.


Kwa upande wao vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu na baadae kuacha ,wamesema homa ya ini imewaathiri baadhi yao kwa kiasi kikubwa kutokana na kuambukizana kupitia damu pamoja na kufanya mapenzi pasipo kutumia kinga hali inayotokana na mwamko duni wa kujali afya zao.

Post a Comment

0 Comments