Business

header ads

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATUHUMIWA KUMI WA UJAMBAZIJeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa kumi wa ujambazi kufuatia msako uliofanywa na jeshi hilo katika msimu huu wa sikukuu ya Eid El Fitri.


Akiongea jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema miongoni mwa watuhumiwa hao yupo mwanamke mmoja ambapo katika msako huo pia wamekamata silaha nane zikiwa ni Bunduki pamoja na Bastola za aina mbalimbali.

Kwa upande mwingine Kamisha Kova amesema jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jiji ilikukabiliana na uhalifu katika sikukuu ya Eid El Fitri ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Waumini wa dini ya Kiislamu nchini Kenya leo wamesherehekea sikukuu ya Idd-ul-Fitr kwa kufanya ibaada katika misikiti na maeneo ya wazi Kaunti ya Mombasa na jijini Nairobi kukamilisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Jana saa nne na robo usiku Kadhi Mkuu Sheikh Shariff Ahmed Muhdhar alitangaza kuwa waumini wa Kiislamu wanaweza kusherehekea Iddi kuanzia leo baada ya kuambiwa na waumini waaminifu kuonekana kwa mwezi.

Kadhi mkuu amewataka waislamu kote nchini kuwa na upendo, uvumilifu, amani na utulivu, salamu alizozitoa kwa maelfu ya waumini waliofurika katika uwanja wa Manispaa ya Mombasa mapema leo katika swala ya Iddi kuashiria kumaliza mfungo wa siku 29.

Post a Comment

0 Comments