Business

header ads

HABARI KAMILI KESI YA WAZIRI PINDA

Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imetupiliwa mbali Kesi iliyokuwa imefunguliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Waziri waziri mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda kuhusiana na kauli aliyoitoa bungeni.


Akisoma hukumu ya kesi hiyo Jaji kiongozi Fakihi Jundu amesema kesi hiyo imetupiliwa mbali kutokana na kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walioorodheshwa waliofungua kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kumfungulia kesi Waziri Mkuu.

Jaji Jundu amesema mahakama imesikiliza pande zote mbili na kueleza kuwa kesi hiyo imeonekana ni batili kutokana na Kinga na Haki za Wabunge,Ibara ya 100 (1) na (2) ambapo kwa mujibu waibara hiyo, kutakuwa na uhuru wa mawazo na majadiliano bungeni, ambao hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote, au katika mahakama yoyote nchini.

Aidha wakili kutoka LHRC,Harold Sungusia amesema ameridhishwa na maamuzi ya kesi hiyo na walifungua kesi hiyo kutokana na kupewa mamlaka na Katiba katika ibara 100 kifungu cha pili kinatoa nafasi kwa mbunge kushitakiwa mahakamani kutokana na kauli zake ndani ya bungePost a Comment

0 Comments