Business

header ads

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAUNGANA NA MKUU WA MKOA, NA MEYA WA KINONDONI KUFANYA USAFI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi
kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) kukagua  mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wakati zoezi la kukagua mto wa Mlalakuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipata wasaa wa kupita na kumpa pole mkazi wa Mikocheni ambaye alikuwa amefiwa na Shemeji yake.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (mbele) akiongozana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kuvuka Mto Mlalakuwa kuongea na wananchi waliokuwa ng'ambo ya mto.
source:michuzi

Post a Comment

0 Comments