Business

header ads

WASANII WA HIPHOP WENYE PESA NYINGI DUNIANI:FORBES


22
Listi maarufu sana ya wasanii wa Hiphop wenye pesa nyingi hatimaye imetoka tena kwa mwaka
2014 na sura zikiwa zilezile lakini kuna waliopanda sana na wengine wameshuka kwenye nafasi zao.1
P Diddy anaweza kuwa msanii wa kwanza wa Hiphop kuwa billionea kwenye miaka michache ijayo kutokana na kasi yake ya kuingiza pesa nyingi na uwekezaji wenye faida kubwa nje ya muziki.
Namba moja kwenye hii listi imekamatwa na P.Diddy ambaye kutokana na mkataba wake mpya na kampuni ya Diageo ambapo bado anahusika na usimamizi wa brand ya Ciroc lakini pia DeLeon Tequila imeongezeka na kuongeza mapato kwake.
Revolt TV anayomiliki P Diddy ambayo imeanza kwa kasi kubwa ndiyo biashara inayosemekana kuwa inaweza kumfanya Diddy kubwa bilionea wa kwanza kwenye HipHop.
Mwaka jana alikuwa na utajari wa dola millioni 580 lakini ndani ya mwaka mmoja ameingiza dola millioni 120 na kufanya utajiri wake kuwa na jumla ya dola za kimarekani millioni 700.
2
Namba mbili ni ya producer na msanii Dr Dre ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani millioni 550.
3
Namba tatu inaenda kwa Jay Z utajiri wake ni dola za kimarekani millioni 520.
4
Namba nne ni ya boss wa YMCMB ‘Birdman’ utajiri wake ni dola za kimarakani millioni 160.
5
Namba tano inamilikiwa na 50 Cent ambaye utajiri wake ni dola za kimarekani millioni 140.

Post a Comment

0 Comments