Business

header ads

ATHARI ZA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA NCHINI TANZANIA

Mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini imesababisha adha mbalimbali zikiwemo kuharibiwa kwa makazi ya watu ,kubomoka kwa madaraja na maafa.
Katika matukio makubwa kuwahi tokea nchini Tanzani kwa kipindi hiki ni lile la kuharbika kwa barabara mkoani Morogoro,kubomoka kwa daraja linalounganisha barabara ya Dar es salaam na bagamoyo na hili la jana la kujaa maji katika barabara kuu katika mkoa wa Pwani eneo la ruvu darajani.
Katika tukio hili lilisababisha kukwama kwa magari ya mizigo na abiria yanaotoka mikoani kuingia Dar es salaam na yanayotoka Dar es salaam kuelekea mikoani.
Takribani masaa 15 yamepotea katika kusubiri maji yapungue katika eneo la ruvu darajani ili kuruhusu upitaji wa magari hayo.
Mtandao huu umeshuhudia msafara wa magari takribani zaidi ya 200 yakisubiri ili kuweza kupita kuendelea na safari.
Aidha rais wa Kikwete akiambatana na mbunge wa Pwani na Chalinze waliweza kufika kuona athari za mvua hizo.
Mamlaka ya hali ya hewa imezidi kuwatahadharisha wananchi kuwa mvua hizi zilizoanza kwa kasi toka tarehe 11 zitaendelea kunyesha mpaka tarehe 14April na kuwataka kuchukua tahadhari mapema.
Swali linabaki je hali hii ya ubovu wa miundombinu  mpaka lini?

Post a Comment

0 Comments