Business

header ads

WALICHOFANYA VIJANA HAWA NI MFANO WA KUIGWA

 Bibi Harusi mtarajiwa Angaja Mwanga akikata keki katika siku ya sendoff yake huko nyumbani m
kwao Dodoma
 Bwana Harusi mtarajiwa Joseph Lymo akivalishwa saa kama zawadi na mke mtarajiwa pale alipopita mbele kutambulishwa
NAPOLEON BONAPARTE, maliki wa Ufaransa wa karne ya 19, alisema hivi wakati mmoja: “Hakuna jambo lililo gumu au lenye thamani zaidi kuliko kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi.” Yaelekea utakubaliana na maneno hayo, kwa kuwa watu kwa ujumla huthamini sana kuwa na uwezo wa kuongoza maisha yao. Wakati huohuo, watu wamejifunza kwamba nyakati nyingine ni vigumu sana kufanya maamuzi.
Hatuwezi kuepuka kufanya maamuzi, yawe rahisi au yawe magumu. Inatubidi kufanya maamuzi kila siku. Baada ya kuamka asubuhi, lazima tuamue tutavaa nini, ni kiamsha kinywa gani tutakachokula, na pia tuamue jinsi tutakavyoshughulika na mambo mbalimbali mchana kutwa. Mengi ya maamuzi hayo si muhimu sana. Mara nyingi hatuyafikirii sana. Ni mara chache tutakosa usingizi hata kama maamuzi hayo ni ya hekima au si ya hekima.
Hivi ndivyo Kijana Joseph Lymo na Angaja Mwanga walivyoamu kufunga pingu za maisha(ndoa) na kuishi kwa raha na furaha, kama nilivyoanza kueleza maamuzi siku hzi vijana wengi wameshindwa kufanya maamuzi kutokana na kutokuwepo na uaminifu na kutokuwa na malengo pindi waanzishapo uhusiano iwe chuoni kazini au mtaani.

Kwa upande mwingine, maamuzi mengine ni muhimu sana. Lazima vijana wengi katika ulimwengu wa sasa waamue ni miradi ya aina gani watakayofuatia. Huenda ikawabidi kuamua watasomea nini na kwa muda gani. Baadaye wengi wao wataamua kama watafunga ndoa au watabaki waseja. Wale wanaotaka kufunga ndoa lazima waamue: ‘Je, nina umri wa kutosha na nimekomaa vya kutosha kufunga ndoa? Ninataka mwenzi wa aina gani, au jambo lililo muhimu zaidi, ninahitaji mwenzi wa aina gani?’ Kuchagua mwenzi wa ndoa ni uamuzi unaoweza kuathiri sana maisha yetu.

Tunapaswa kufanya maamuzi ya hekima kuhusiana na mambo muhimu, kwa kuwa furaha yetu inategemea sana maamuzi tunayofanya. Huenda wengine wakahisi kwamba wana uwezo wa kufanya maamuzi hayo na huenda wakakataa kusaidiwa.Mtandao huu unawatakia maharusi watarajiwa heri na mafanikio katika maisha ya ndoa yatakayoanza kuanzia tarehe 22/02/2014.

Bi harusi mtarajiwa akikabidhi keki kwa wazazi
Bi harusi mtarajiwa akikabidhi keki kwa wakwe

Post a Comment

0 Comments