Business

header ads

BAJ WA VIPAJI WAANDIKA HISTORIA IRINGABAJ wakikabidhiwa mbuzi na Rais wa Chuo
Timu iliyoingia fainal na kuandika historia BAJ
 Mveterani mwana BAJ wa enzi hizo Godwin Gondwe akiongea na wanabaj baada ya ushindi

Sikuwahi pata nafasi ya kuandika habari za michezo  wala kuchambua soka, sio kwamba sikupewa nafasi ni kwasababu nyingi sana ambazo hazielezeki ila kwa leo nimepata nafasi ya kuwa mchambuzi kama walivyo wengine akina Musaa Kawambwa, Omari Mtamike, Lazaro na wengine wengi ambao uwezo wao wameupata toka kitivo cha BAJ WA VIPAJI.


Kwa miaka mingi kumekuwa na mashindano ya michezo baina ya vitivo mbalimbali katika chuo kikuu iringa zamani Tumaini Iringa maarufu kwa jina Interfaculty. Yamekuwa na ushindani mkubwa Katik a mpira wa pete, wa miguu, na wa mikono usishangae mingine siijui maana haijaanishwa na kupewa nafasi kama michezo rasmi najua frank kimaro utaanza cheka.

Katika historia ya miaka mingi kupita katika mashindano hayo hapo chuoni timu ya Kitivo cha habari BAJ imekuwa ikisuasua sana katika uwakilishi wake katika sehemu zote tajwa za ngazi ya kimichezo na mara nyingi kujikuta wanakuwepo  katika mpira wa miguu ila kwa bahati mbaya kutolewa katika kipindi cha mwanzo kabisa.

Nakumbuka mwaka 2009 nikiwa mwaka wa kwanza chini ya uangalizi wa kocha mkuu Mwl Julius Mtemahanji akisaidiana kwa karibu na swahiba wake Aloyce Godfrey kwa bahati nzuri au mbaya mimi waliniteua kipa nikisaidiana na Habakuki Urio najua utacheka maana matokeo yake wayajua yalikuwa ni yepi.
Historia iliwekwa kwa mara zote kushika mkia na kuambulia kupongezwa kama timu washirika na mara nyingine waliitaja timu ya BAJ  kama timu yenye nidhamu kwa kipindi chote cha mashindano kiukweli sababu zilikuwa nyingi mbali na kufungwa haikuwahi kata tamaa ya kuishia njiani mpaka mtoano ulipofika.

Ukweli ni kwamba nikitaka andika nitaandika mengi ila kwa leo niishie hapa nikitoa pongezi kwa timu ya kitivo cha habari BACHELOR OF ARTS IN JOURNALISM na uongozi mzima kwa kuhakikisha kuwa hadhi imerudi kwa kuwa mabingwa wa mpira wa miguu mwaka 2013/2014.

Ama kweli kikosi hiki kilichotinga fainali pamoja na timu ya IT na kukwapua ubingwa  kwa kufunga goli 3 -1, kiliundwa na Chacha Fred,Hija Zakaria, Osca Galus, Mike Omben,Frank, Najim, Maila, Jerry, Lazaro, George, Hussein. Natoa pongez zangu kwa hili naamini ubingwa huu hautaenda kwa mwingine katika historia ya soka chuo cha Iringa. By E. Materu former BAJ member

Post a Comment

1 Comments

  1. Thanx Materu tuko pamoja ni kweli tulijiuliza kwa muda mrefu lakin yametimia na huu ni mwanzo, sasa heshima mtindo mmoja.

    ReplyDelete