Business

header ads

WEMA SEPETU AMUOKOA KAJALA KWENDA JELA

Wadau wa tasnia ya filamu nchini wamemvulia kofia mlimbwende na mcheza sinema maarufu nchi Wema Sepetu baada ya kumuokoa msanii mwenzake Kajala Masanja asiswekwe gerezani baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13 iliyohitajika baada ya hukumu iliyokuwa inamkabili Kajala na mumewe Faraji Agustino kwa kupatikana na makosa ya kutakatisha fedha haramu (money laundering). 

 Mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam Kajala alikuwa keshahukumiwa kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5, ama kutoa faini ya shilingi milioni 13.

 Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu. Baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakamani hapo, Wema Sepetu alijitolea kulipa faini hiyo ya shilingi milioni 13 na kumuokoa Kajala asitumikie adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 gerezani. 

 “Hata sifahamu kwa nini watu wanamsema vibaya mtu mwenye roho kama hii aliyonayo Wema (Sepetu) ”, alisema Masudi Bitebo, mla vichwa (kinyozi) maarufu anayetamba katika anga za Mwananyamala B kwenye saluni yake ya Bitebo Jnr Hair Designer, ambako ndiko mwanadada Wema Sepetu hutengenezwa nywele zake. 

Mdau mwingine, Mwarami Popati wa Tabata, amesema kwamba Mola atamlipia Wema Sepetu kwa wema wake, pamoja na kujali maslahi yaw engine. “Piga ua lakini Wema (Sepetu) ni bonge la staa hapa Tanzania. “Ustaa ujue unaanzia moyoni. Haya ya nje ni mwili tu. Wasanii wangapi wanaotengeneza fedha nyingi walikuwepo mahakamani leo. Lakini ni wangapi walijitokeza kumuokoa mwenzao?” alisema Popati.

Kwa habari ya kina ya kesi hii mtembelee mwanalibeneke wa habari za mahakamani Happiness
Kajala na mumewe kabla ya hukumu kusomwa leo
Mzee Masanja na baadhi ya wasanii wakitahayri baada ya hukumu
Kajala amwaga chozi baada ya hukumu
Wema Sepetu akiondoka  na Kajala baada ya kumlipia faini ya milioni 13
Mratibu wa shughuli za kumuokoa Kajala, Dokta Sheni akiwa na Kajala baada ya kuachiwa huru.
Picha zote na GPL

Post a Comment

0 Comments