Business

header ads

UNDANI WA HABARI YA KUUWAWA KWA DEREVA WA BODABODA TANANGOZI IRINGA HUU HAPA


Katika tukio la kusikitisha mwili wa marehemu sadiki mbwilwa (26) umekutwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani huku ikisadikiwa kupigwa na kitu chenye ncha kali pamoja na fimbo ya muanzi.

Akielezea kuhusu kifo hicho baba mdogo wa marehemu carlos simoni Mbwilwa ameeleza kuwa marehemu aliondoka nyumbani kwake muda wa saa bili baada ya kupigiwa simu na watu aliowafahamu kuwa ni abiria wake waliomtaka awapeleke katika eneo la wenda ipamba katika mkoa wa Iringa. Lakini kwa bahati mbaya walipofika katika kijiji cha wemba mafuta yaliisha na ndipo ilipombidi marehemu kwenda kununua mafuta lita moja na aliporudi ndipo alipovamiwa na abiria hao na kasha kumvuta kichakani na kumtendea unyama huo.

Baba mdogo wa marehemu anaendelea kueleza kuwa kutokana na  kutoonekana kwake kwa usiku huo marehemu ambaye alikuwa na kawaida ya kurudi nyumbani ndipo alipo mama wa marehemu alipotoa taarifa na jitihada zikamfikia mtendaji wa kijiji.
Mtendaji wa kijiji  cha Tanangozi Lucy Msigwa anaeleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo aligonga kengele na wananchi wakakusanyika na walipojiuliza maswali wakaamua kuelekea eneo la Ipamba ambapo marehemu alikuwa akiepeleka abiria mara nyingi na walipofika karibu na mto katika kijiji cha wenda ndipo walipoiona element(kofia ya pikipiki) lakini mwili wa marehemu haukuonekana wala pikipiki.
Anaendelea kueleza kuwa usiku wa kuamkia jana juhudi za kumpata ziligonga mwamba na kuacha taarifa kwa wanakijiji cha wenda ambao asubuhi ya leo ndipo walileta taarifa ya kuuona mwili wa marehemu ukiwa katika majeraha mengi kichwani.
“Nimepoteza kijana mwenye kujituma asiye na shida na mtu na mwenye utayari wa kufanya kazi na nadhani amekufa kutokana na utayari wake maana mda huo angeweza sema amechoka, tukio hili ni la kwanza kutokea toka niingie uongozini naomba Polisi waliangalie suala hili ili kuleta na ushirikiano na haswa pale wanapohitajika kufika katika eneo la tukio” alisema

Kwa mujibu wa shuhuda dereva mwenzake wa bodaboda Solomoni  Ujengo anasema mwili wa marehemu sadiki ulionekana ukiwa umepigwa na kitu kizito pamoja na tofali la kuchoma na kukilaani kitendo hicho kwani katika kufanya kazi na marehemu hakuwahi kuwa na tatizo na mtu yeyote na alikuwa na ushirikiano na kuliomba jeshi la polisi kufuatilia waliotenda unyama huo na kutiwa nguvuni.

RIPOTI TOKA KWA DAKTARI NA POLISI INASEMAJE?
Baba mdogo wa marehemu Carlos Simon anaeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa na kuonesha kuwa marehemu alipigwa na kitu chenye uzito katika kichwa na kusababisha umauti wake na huku taarifa zikiwa tayari zimefika polisi na kueleza kuwa baada ya kupeleka namba ya marehemu katika ofisi ya Vodacom ndipo ilipogundulika kuwa marehemu alipigiwa simu katika muda wa saa mbili na nusu usiku na kwamba upelelezi kubaini wahusika walipo unaendelea.

Aidha Simon amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo mpaka watu hao waliotenda unyama huo kubainika na kutiwa nguvuni.
Marehemu amemuacha mke ambaye kwa mujibu wa taarifa alimuoa mke huyo muda wa wiki moja iliyopita na kuacha maswali mengi kwa watu waliomfahamu na ndugu kuhusu kifo hicho.

Madereva wa bodaboda wakiendelea na shughuli katika kjiji cha Tanangozi Iringa leo
MTANDAO HUU UNAPENDA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA AMEN.

Post a Comment

0 Comments