Business

header ads

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI DAUDI MAWNGOSI AMEFARIKI DUNIA KATIKA VURUGU ZA CHADEMA

Habari za hivi punde; Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi, pichani - amefariki dunia kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa chama cha Chadema.Habari zilizotufikia kutoka huko, zinadai kuwa Mwangosi, ambaye ni mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel ten, amefariki papo hapo. 

Mwangosi alikuwa ni mmoja ya waandishi wa habari nane (8) waliokuwepo katika msafara wa mkutano wa CHADEMA. Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa Mwangosi amedondokewa na Mabomu la machozi  yaliyorushwa na Polisi na kumfikia yeye ambapo alifariki hapo hapo.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU  DAUDI MWANGOSI MAHALI PEMA AMEN.


Mtandao huu utazidi kukupatia habari zaidi na picha kuhusu tukio lenyewe.


Post a Comment

0 Comments