Business

header ads

MTIHANI WA DARASA LA SABA IRINGA WAFANYIKA PASIPO NA KIKWAZO
Wanafunzi 3169 wa darasa la saba Mkoani Iringa leo wameungana na watahiniwa wengine kote nchini kote katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi.

Huku wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri na kuvuka salama katika kipimo hicho ambacho kitatoa tathmini ya kile ambacho wamekuwa wakifanya kwa kipindi cha miaka saba.

Mitihani hiyo ya siku mbili inahusisha zaidi ya wanafunzi laki nane nukta tisa na unahusisha masomo ya Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii ambapo leo wamefanya mtihani wa sayansi,hisabati na Kiswahili.

Afisa Elimu wa manispaa ya Iringa bwana Anjelus Kisiga  amesema jumla ya watahiniwa 3169 wanafanya mtihani katika manispaa ya iringa na kati yao wasichana ni 1626 na wavulana 1543 katika shule za msingi 47.

Akiongelea kuhusu kuwa mfumo mpya wa mtihani wa mwaka huu kisiga amesema hawana shaka nao kwani mfumo huo umetolewa Mafunzo ya kutosha kwa maafisa elimu, walimu wakuu, waratibu elimu kata na walimu wa taaluma kuanzia mwezi februari hadi Agosti mwaka huu.

Nao wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani hapa wameendelea kufanya mitihani yao kwa utulivu huku kukiwa na usimamizi pamoja na ulinzi wa kutosha katika vyumba vya mitihani licha ya walimu wa shule kadhaa kushindwa kutoa maoni yao kuhusu mfumo mpya wa mitihani hiyo.

Kwa mara ya kwanza hapa nchini Mtihani wa darasa la saba mwaka huu unafanyika kwa kutumia teknolojia mpya ya ‘Optical Mark Reader’ (OMR), ambapo watahiniwa watatumia fomu maalum katika kujibu maswali na yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta, ambapo kwa mwaka huu wavulana watakao fanya mtihani huo ni 426,285 sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni 468,596 sawa na asilimia 52.36.

Veronika chipeta ni mwanafunzi wa shule ya msingi mkombozi anasema kuwa mtihati kwake ulikuwa rahisi na anatarajia kufaulu wazazi wake wajiandae tu kwaajili ya kumpeleka kidato cha kwanza.

Kwa upande wa Gwamaka Saul kutoka shule ya msingi ya Mlandege anasema mitihani yote ilikuwa ya kawaida japo mtihani wa sayansi kwake haukuja kama alivyotarajia na kusema hilo haliwezi kumfanya asifaulu vizuri.

Mitihani hiyo inatarajiwa kumalizika siku ya kesho, swali je? Kutumika kwa walimu kutoka shule za sekondari kusimamia mitihani zaweza kutatua tatizo la kuigiliziana na kufaulu kwa watoto wasiojua kusoma au kuandika?Post a Comment

0 Comments