Business

header ads

BALOZI WA MAREKANI AZINDUA MKAKATI WA KUPAMBANA NA UKIMWI IRINGA

Balozi wa Marekani Alfonso E. Lenhardt akiwahutubia wananchi wa Iringa
Balozi wa Marekani Lenhardt akihutubia
Maambukizi ya Ukimwi Mkoni Iringa  yanakadiriwa kuwa 15.6 % na  ni ya juu kabisa nchini ambayo ni mara tatu ya wasatani wa Kitaifa.
Mradi wa TUNAJALI rejea katika tiba jail afya yako umedhamilia kupambana na maambukizi hayo pamoja na kutokomeza kabisa kufikia lengo la kuandikisha na kasha kuwabakiza kwenye huduma na tiba za VVU/UKIMWI zaidi ya watu 20000 wanaoishi na virusi hivyo ili waweze kusihi maisha yenye afya na tija zaidi.
Hayo yamezungumzwa na Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt katika uzinduzi wa mkakati wa “rejea kwenye tiba “ uliofanyika leo katika kituo cha Afya Ipogolo Manispaa ya Iringa.
Alisema hivi sasa asilimia takribani 25% ya watu waliokuwa wakitumia ARV wameacha tiba hiyo ambayo ni muhimu na siyo tu  kuwaanzishia watu dawa lakini ni muhimu pia kuhakikisha kuwa wagonjwa hao wanabaki katika tiba.
“Kiwango hiki cha walioacha dawa kinatutia wasiwasi kuhusu afya na ustawi wa watumiaji na pia kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi katika jamii kwa ujumla,” alisema Lenhardt.
Kwa mujibu wa mwongozo wa huduma na tiba za VVU na UKIMWI uliofanyiwa marekebisho na kutolewa na Serikali ya Tanzania mapema mwaka huu ambapo kwa sasa mtu anastahili kuanza kutumia ARV wakati CD4  zake zikiwa 350 badala ya 200.
Alisema uzinduzi wa Mkakati huo ni madhubuti kwa kueneza ujumbe wa “pima , endapo umeambukizwa na unastahili kuanza tiba ni vyema ukaanza mapema na endapo umeacha tiba kwa sababu yoyote ile, ni lazima ukarejea kwenda kupata huduma”.
Baadhi ya wananchi wa Iringa waliohudhuria kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika kiuo cha afya Ipogolo

 Aidha Balozi huyo amesema katika kipindi cha miaka tisa toka 2003 watu wa Marekani kupitia PEPFAR wamewekeza dola za Kimarekani Bilioni 2 kwa ajili ya kupambana na VVU na UKIMWI nchini Tanzania ambao ni uwekezaji katika maisha.
Kwa mujibu wa taarifa ya mapambano dhidi ya Ukimwi Mkoani Iringa kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 ambapo Iringa imeathirika kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na Mikoa mingine Tanzania ambapo utafiti unaonyesha maambukizi ya VVU na janga la UKIMWI kitaifa uliofanyika mwaka 2007/2008 maambukizo yameongezeka kutoka asilimia 13.4% mwaka 2003/2004 na kufikia asilimia 15.7.
Aidha hatua ya mkakati huo imewezesha Watanzania zaidi ya 300,000 kutumia dawa zinazopunguza makali ya VVU  ambapo hivi sasa zaidi ya Watanzania 525,000 hupokea matunzo na huduma mbalimbali zikiwemo huduma za majumbani.

Post a Comment

0 Comments