Business

header ads

TBL YAFUNGUA MRADI WA VISIMA UNAOGHARIMU MIL 39

Jiwe la msingi
Meneja wa masoko TBL Iringa Raymond Degera akizungusha pampu ya maji ili kujaza ndoo
Mkurugenzi CSR TBL akinywa maji kuonesha ni safi na salama kwa matumizi yote.
Mama mkazi wa Kata ya manda akitwisha ndoo na Kilindo TBL pamoja na mgeni rasmi ya maji ishara ya kuwa mradi umefunguliwa rasmi.Kwanza kushoto Mratibu wa Mradi Cannon John Kwetu katikati mgeni rasmi Meneja wa masoko TBL katika mkoa wa Iringa, Njombe na Songea Raymond Degera wa pili kushoto ni Mkurugenzi toka TBL Steven Kilindo
Mkurugenzi wa Corporate Affairs toka TBL Steven Kilindo akimpongeza mgeni rasmi
Muwakilishi wa mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya Ludewa Afisa tarafa akifungua mradi huoWapiga ngoma wakipiga ngoma ya asili aina ya Malahamisi
Afisa mtendaji wa kata ya Luguli akiongea na wanahabari kuhusu kufunguliwa kwa Visima 15

WANANCHI wa kata ya Manda na Luguru kupitia ufadhili wa kampuni ya bia TBL leo wameweza kuachana na adha ya maji iliyokuwa inawasumbua kwa kipindi kirefu sana.
Wakazi hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia ziwa nyasa kupata maji kwa mahitaji yao mbalimbali ya nyumbani na katika shughuli za ujenzi ikiwa ni umbali wa masaa 3 kwenda na kurudi ili kupata huduma hiyo ya maji.
TBL ikiwa ndio kampuni ya kwanza kufika katika kijiji cha mmanda na kufanikiwa kufungua visima 15 ambavyo vitaondoa adha iliyokuwepo kwao.
Mradi huo wa maji uliogharimu kiasi cha shilingi mil 39, Mradi ambao ulianza mwezi wa 9,2011 unawanufaisha wakazi wa kata mbili ya Manda na kata ya Luguru na unafaidisha vijiji sita ambavyo ni Kipingu, Ngelenge,Ilela, Msungu, Digalo na Mbungu.
Kata ya Manda inakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya 6000 ambao wengi wao wanategemea ziwa nyasa katika kuwasaidia kupata huduma hiyo muhimu ya maji. Akiongea na mtandao huu Daktari wa Zahanati ya kijiji cha Ngelenge Leonard Lukuwi amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakiteseka sana na magonjwa ya kuhara na Typhod kutokana na maji ya mto Luhuu kuwa machafu na yanapatikana kwa umbali wa zaidi ya kilometa nne. Nakuongeza kuwa toka TBL wamechimba visima hivyo tatizo hilo kwa sasa limepungua kwa asilimia 75.
Naye Ofisa mtendaji wa kijiji cha ngelenge James Mapunda amesema wananchi walikuwa wakienda kwa umbali wa zaidi ya masaa mawili katika mto Luhuu ambao pia umepoteza maisha mengi ya watu kutokana na kuvamiwa na mamba. Aliongeza kwa kuishukuru TBL kwa kusogeza huduma karibu ambayo itasaidia wengi na kupunguza idadi ya vifo vilivyokuwa vikitokana magonjwa kama kuhara na Typhod.
Rev Cannon John Kwetu ni mratibu wa mradi huu kutoka shirika la SouthWest Tanganyika anaelezea kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Ilela na amekuwa akiona wananchi wakipatwa na matatizo mengi ndipo alipoamua kuomba kwa kampuni ya TBL na walikubali na kuweza kujenga visima 15. Kwetu ameongeza toka mradi huo uanze mwaka 2011 tatizo la magonjwa ya mlipuko limepungua kwa asilimia 75 na kubakiwa na 25 ambazo anaamini wananchi wakizingatia suala la afya na kutumia maji hayo safi tatizo hilo litatokomea kabisa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mradi huo mwakilishi wa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Ludewa ameeleza afisa tarafa Mwambeleko ameishukuru TBL na kuwataka wananchi kuuendeleza mradi huo na kuzitaka kampuni nyingine kuiga mfano wa kamuni hiyo ili kuboresha maisha na kuleta maendeleo haswa katika maeneo ya vijijini ambayo yamesahaulika.
Amewataka wananchi kutumia vizuri visima hivyo kwa faida ya wote si kwa kuangalia serikali na TBL itawasaidiaje bali wafahamu kuwa ni wajibu wao kuvilinda na kuvitunza ili kuweza kuwasaidia kwa sasa na baadae.
Mkurugenzi wa Corporate affair TBL Steven Kilindo akizunguza kwa niaba ya kampuni ameeleza kuwa kampuni imeziimia kurudisha shukurani kwa jamii bila kujali ni watumiaji wa bidhaa zao na kuhakikisha wanafanya jitihada zao kuhakikisha kuwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya Tanzania wanapata huduma muhimu haswa ya maji. Mbali na hayo Kilindo ameishukuru serikali na wananchi kwa kutambua umuhimu wa kampuni ya TBL na kushirikiana nao ili kufanikisha kuwepo kwa visima hivyo.
“Serikali imetupa mazingira mazuri ya kibiashara na kutokana na hilo basi nasi kwa kutambua hilo tumeamua kuisaidia serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo kuleta huduma ya maji kwani maji ni uhai” alisema
Pia aliwataka wananchi kwa kutambua umuhimu wa huduma ya maji kuwa waangalifu na kutunza mradi na kuufanya endelevu na kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji kwani maji yanapungua kutokana na kutotunzwa kwa vyanzo hivyo.

Post a Comment

0 Comments