Business

header ads

MATUKIO YA LOVE TANZANIA FESTIVAL UWANJA WA JANGWANI
Vijana walioongozana na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na mafundisho ya dini kwa njia muziki.
Umati wa watu ukiwa kwenye foleni ya kupata huduma ya chakula uwanja hapo.
Michezo ya pikipiki.


Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wakishuhudia mchezo wa Baiskeli.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd akihakikisha swala usafi linazingitiwa uwanjani hapo kama inavyoonekana.
Mchezo wa kuruka na baiskeli ambao pia uliwaacha watu midomo wazi, picha kwa hisani ya Issamichuzi blog.
Masanja Mkandamizaji jukwaani akimsifu Mungu wake.
Askofu Andrew Palau akitoa ujumbe wa neno la Mungu.
Don Moen akiwa jukwaani kumtukuza Mungu.
Don Moen akiendelea kumsifu Mungu katika sherehe hizo.
Mwanadada Nicole C. Mullen akiwa jukwaani, aliweza kuwabariki watu alipoimba wimbo my redeemer lives kwa kiswahili. .

Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam hapo jana waliweza kufurika katika viwanja vya Jangwani jijini   hapa ili kupata baraka zao katika sherehe za Ipende Tanzania (Love Tanzania Festival) inayoongozwa na muhubiri Andrew Palau akishirikiana na waimbaji kutoka ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Don Moen na mwanadada Nicole C. Mullen ambao wameweza kuwabariki wengi kwa huduma yao.

Katika siku ya kwanza hapo jana watu walipigwa butwaa kuona mchezo wa kuruka na pikipiki, uimbaji na muziki kwa ujumla hasa wakati walipoimba waimbaji Nicole na Don Moen vyombo viliweza kusikika vyema kabisa, sherehe hizo zinatarajiwa kuhitimika hii leo katika viwanja hivyo vya Jangwani kuanzia majira ya saa saba mchana hadi saa 2 usiku.

Post a Comment

0 Comments