Business

header ads

MAANDALIZI SHEREHE ZA LOVE TANZANIA FESTIVAL YAKAMILIKA

Wakati lile tamasha la sherehe la Love Tanzania Festival linatarajiwa kuchukua nafasi hapo kesho katika viwanja vya Jangwani, maandalizi yake yako ukingoni kabisa kwa wanamuziki kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kuvijaribu vyombo ambavyo vitatumika hiyo kesho na jumapili.

Tamasha hilo ambalo litaongozwa na mtumishi wa Mungu Andrew Palau tayari limekuwa gumzo jijini Dar es salaam kutokana na ushirikishwaji watu mbalimbali katika huduma za kiroho na kiwmili ikiwemo huduma ya watu kupewa miwani bure, pia wanafunzi katika baadhi ya shule jijini Dar es salaam wamebahatika kusikia neno la Mungu pamoja na kujionea michezo mbalimbali ikiwemo ya kuruka na baiskeli.

Ambapo taarifa zinasema mwimbaji maarufu wa muziki wa gospel duniani Don Moen  tayari ametua jijini Dar es salaam na timu yake huku waimbaji wengine kama Dave Lubben, Nicole C. Mullen na waimbai wengine kutoka nchini wanatarajiwa kuungana pamoja kumsifu Mungu katika sherehe hizo za Love Tanzania Festival.

            HAPA BAADHI YA PICHA YA MAMBO YANAVYOKWENDA

               

Post a Comment

0 Comments