Business

header ads

CHADEMA IRINGA WAEPUSHA SHARI NA FFU

kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda (kushoto) akiwa na askari wake eneo la uwanja wa Mwembetogwa jioni hii

Viongozi wa Chadema wakizunguka mtaani jioni hii

JESHI la polisi mkoa wa Iringa na chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wasumbuana kwa zaidi ya masaa 10 leo katika harakati za kuzuia mkutano wa chama hicho.
Chadema na polisi walijikuta katika mvutano mkali na kuzungushana huku na kule leo baada ya viongozi wa Chadema mkoa wa Iringa kushikilia msimamo wao wa kuwepo kwa mkutano huo katika viwanja vya mwembetogwa pamoja na jeshi la polisi kuzuia mkutano huo.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano huo mkali baada ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiongozwa na kamanda wake Mnunka wakitanda eneo la uwanja wa mkutano eneo la Mwembetogwa huku viongozi wa Chadema wakizunguka huku na kule mjini Iringa kushinikiza mkutano huo.
Mbali ya askari hao kumwagwa eneo la uwanja wa Mwembetogwa na hata kuzuia wafanyabiashara ndogo ndogo eneo hilo kuondoka ,bado idadi kubwa ya askari walionekana wakizunguka maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa huku baadhi yao wakiwa wametanda nje ya ofisi ya Chadema wilaya ya Iringa mjini eneo la Mshindo kama njia ya kuzuia viongozi hao kutoka kwa maandamano eneo hilo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao (Chadema) ambaye pia ni mjumbe kamati kuu Taifa alisema kuwa kutokana na mvutano huo wa jeshi la polisi na Chadema wameamua kutoufanya mkutano huo leo
Abwao alisema kuwa kutokana na hoja hiyo ya polisi ya kuwa kwa sasa ni zoezi la sense ya watu na makazi wamelazimika kutii agizo hilo na hivyo kuamua kusogeza mbele mkutano huo.
Hata hivyo alisema baada ya jeshi la polisi kutangaza kusitisha mkutano huo kwa upande wake alilazimika kutangaza katika vyombo mbali mbali vya habari zikiwemo radio za mkoa wa Iringa ili kusitisha mkutano huo japo tayari kulikuwepo na maandalizi makubwa ya mkutano huo.
Hata hivyo Abwao aliwaomba radhi wananchi wa jimbo la Iringa mjini ambao walikuwa tayari kushiriki mkutano huo na kuwaomba wajiandae kwa wakati mwingine ambao chama hicho kitatangaza mkutano huo .
"Chadema tumetumia busara kuepusha shari zaidi kati ya polisi na chama pia kuepusha wananchi kumwaga damu"
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alieleza sababu za kuzuia mkutano huo kuwa ni baada ya kupokea agizo kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini hasa baada ya tukio la Morogoro jana
Hivyo alisema kwa sasa wakati zoezi la sense linaendelea chama chochote cha siasa hakitaruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara hadi hapo zoezi hilo la Sensa litakapokamilika.

Post a Comment

0 Comments