Business

header ads

TASWIRA ZA MAJERUHI WA MELI YA MV SKAGIT JANA

...Huduma za matibabu zikiendelea.…
Mmoja wa majeruhi wa ajali ya Boti ya Seagul iliyozama katika eneo la Pungume karibu kilomita 48 kutoka Bandari ya Zanzibar jana, akipata matibabu.
 MELI YA MV SKAGIT ikiwa imezama
Kwa mujibu wa Waziri Emmanuel Nchimbi  wakati akiongea na TBC1 amesema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”

MUNGU AZILAZE PEMA ROHO ZA MAREHEMU AMEN NA AWAPE FARAJA WAFIWA WOTE.


Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama jana katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31. Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo. SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar. Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kutoka kwa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy. Chanzo:www.francisgodwin.blogspot.com

Post a Comment

0 Comments