Business

header ads

MKUU WA MKOA WA IRINGA AWEKA SULUHU NA WAANDISHI WA HABARI

 Mkuu wa mkoa Dr Christine Ishengoma akizungumza na waandishi wa habari wa Iringa
Hapa akisistiza jambo kwa baadhi ya wanahabari waliofika katika ofisi yake ili kupata muafaka wa mgogoro waliokuwa nao baina yao na ofisi ya mkoa.
 Mweyekiti wa IPC Mwangosi akiongea jambo mbele ya mkuu wa mkoa wakati alipokutana na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoa wa Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma amevunja ukimya na kuongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa. Nakuwataka kushirikiana vyema kama ilivyokuwa awali na kuandika habari zinazohusu mkoa wa Iringa.

Dkt. Ishengoma ameongeza kuwa wanahabari ni watu wa muhimu sana katika jamii na kuwataka kutumia taaluma yao katika kuelimisha jamii hasa kuhamasisha wananchi kushiriki katika sensa ya watu na makazi ambayo itaanza mwezi August 26 mwaka huu.

Akishukuru kwa niaba ya wanahabari Iringa mwenyekiti wa Iringa Press Club(IPC) Mwangosi amefurahishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa kuwaita na kutaka suluhu ili kuendeleza ushirikiano na kuleta maendeleo katika mkoa wa Iringa. Pia amewataka waandishi wa habari kuridhia muafaka huo na kuendelea kufanya kazi kama maadili ya taaluama ya habari yanavyoelekeza.

Post a Comment

0 Comments