Business

header ads

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MADAKTARI WALIOGOMA,AWAFUTA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA MGANGA MKUU WA SERIKALI
Waziri Mkuu,Mh.Mizengo Pinda amesema kuwa amewafuta kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Deo Mtasiwa kuanzia leo hii kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro huo ambao umekuwa ukisababisha matatizo makubwa kwa Taifa

Waziri Mkuu amewataka Madaktari waunde kamati maalumu ambayo itakusanya mapendekezo ya madaktari wote na kumpelekea yeye ili aweze kuyafanyia kazi,huku akiwataka Madaktari hao kurudi kazini na kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa hapo awali

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Hawa Ghasia na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela

Baadhi ya madaktari na wauguzi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Post a Comment

0 Comments