Business

header ads


WAVUVI WA SAMAKI WA MAGUFULI JELA MIAKA 20

Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imetoa hukumu ya miaka 10 & 20 kwa raia watano wa CHINA wa kesi maarufu iliyopewa jina la ‘”SAMAKI WA MAGUFULI’ ambapo pamoja na hukumu hiyo mahakama hiyo imetaifisha Meli waliyokamatwa nayo.

Jaji Augustino Mwajira amesema kwa kuzingatia hoja za wakili wa utetezi na za upande wa utetezi ameamua kuitaifisha meli hiyo kwa manufaa ya umma ili kukomesha uvuvi haramu kwenye ukanda wa Tanzania”

Kuhusiana na washitakiwa katika shitaka la kwanza amewahukumu nahodha wa meli hiyo na wakala wa meli hiyo kulipa faini ya shilingi bilioni moja au kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja.

katika shitaka la pili mahakama kuu imemtia hatiani nahodha wa meli hiyo kwa kuongoza meli isiyotambulika na kumuhukumu kwenda jela miaka kumi au kulipa faini ya shilingi bilioni 20 ambapo hata hivyo washitakiwa wameruhusiwa kukata rufaa huku Watuhumiwa wengine watatu waliokua wanatetewa na wakili wa kujitegemea wameachiwa huru baada ya mahakama kuwaona kwamba hawana kesi ya kujibu.

Post a Comment

0 Comments